Tuesday, March 24, 2015
10:15 AM
| Posted by
Unknown
|
Meneja wa kiwanda cha Bia cha TBL Mbeya, Waziri Jemedari akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya(hawapo pichani) walipofanya ziara na kushiriki shindano la kuonja bia hivi karibuni.
Meneja mawasiliano na Uhusiano wa TBL, Editha Mushi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari Mbeya.
Meneja wa Kiwanda cha Bia Waziri Jemedari akitoa zawadi kwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten, Saada Matiku baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika shindano la kuonja bia ambapo alipata alama zote tano.
Meneja mauzo na usambazaji nyanda za juu kusini VIvianus Rwezaura, akimkabidhi zawadi Keneth Ngelesi ambaye aliibuka mshindi wa pili kwa kujikusanyia alama nne kwa tano.
Meneja viwango wa TBL Esther Mmari akimkabidhi zawadi Merali Chawe mwandishi wa gazeti la Daily news ambaye alikuwa mshindi wa tatu katika shindano la kuonja bia baada ya kujikusanyia alama tatu kwa tano.
Washindi wakiwa na zawadi zao.
Mwakilishi wa gazeti la Tanzania daima Mbeya, Christopher Nyenyembe akijaza fomu ya mashindano.
.Mtangazaji wa redio ya Mbeya fm Fredy Jackson (kushoto) akiuliza maswali kutoka kwa Saada Matiku ambaye alikuwa mshindi wa kwanza lakini bado alipata sifuri.
Mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo, Joackim Nyambo akiwa sambamba na Mmiliki wa mtandao wa Mbeya yetu, Joseph Mwaisango wakifuatilia kwa makini katika mashindano ya kuonja bia.
Waandhishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya wakiwa kwenye chumba cha mashindano ya kuonja bia.
Meneja rasilimali watu George Albano akitoa somo kwa waandishi wa habari mkoa wa Mbeya
Waandhishi wa habari Mbeya wakipata maelezo mbali mbali kuhusiana na kiwanda cha bia cha TBL.
.Waandishi wa habari Mbeya wakielekea kutembelea mitambo ya kuzalisha bia kiwandani hapo.
.Meneja wa Kiwanda akitoa maelekezo.
Waandishi wa Habari wakipata maelekezo mbali mbali juu ya uzalishaji wa bia.
Baadhi ya Wataalamu wa Kiwanda cha Bia cha TBL wakiendelea na majukumu yao.
Muonekano wa Kiwanda
Picha ya pamoja baada ya kumaliza Ziara.
WAANDISHI wa Habari Mkoa wa Mbeya hivi karibuni walifanya ziara ya kutembelea kiwanda cha bia TBL Mbeya ambapo pia walipata nafasi ya kushiriki mashindano ya kuonja bia.
Katika shindano hilo, Mzoefu Saada Matiku ambaye ni mwandishi wa Chanel Ten aliibuka kidedea kwa kupata alama tano kwa tano ikiwa ni mara ya pili tangu apate nafasi kama hiyo kwenye mashindano ya mwaka juzi.
washindi wengine ni Kenneth Ngelesi wa Tanzania Daima aliyeibuka mshindi wa pili huku Merali Chawe wa Daily news akiibuka kidedea katika nafasi ya tatu.
Mbali na mashindano hayo Uongozi wa Kiwanda hicho umeilalamikia Serikali kwa kitendo cha kupandisha ushuru kwenye vinywaji katika kila mwaka wa bajeti jambo linaloathiri uzalishaji kwa makampuni binafsi.
Hayo yalibainishwa na Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Kiwanda cha Mbeya, Waziri Jemedari, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari walipofanya ziara kiwandani hapo Iyunga jijini Mbeya.
Jemedari alisema uzalishaji wa bidhaa zao katika kiwanda cha Mbeya umepungua kutokana na ongezeko la Kodi ambapo awali kabla ya kupandishiwa kwa kodi hiyo Kiwanda kilikuwa kinafanya kazi masaa 24 kwa siku 7 lakini sasa kinafanya kazi masaa 24 kwa siku tatu.
Alisema hadi sasa uzalishaji huo umepungua kwa asilimia 40 ambapo wakati mwingine hulazimika kuzima na kupumzisha mitambo sababu kubwa ni kupungua kwa mauzo baada ya bei kuongezeka.
Alisema uzalishaji ulikuwa ni Hektolita 12000 hadi 6000 kwa siku lakini sasa hivi umeshuka hadi Hektolita 400 hivyo kusababisha hata kutishia kupunguza watumishi.
Alisema kitendo cha serikali kupandisha bei kwa mlaji kinaathiri pande nyingi ambapo Mlaji mwenyewe nashindwa kumudu gharama za kununua bidhaa ili hali mzalishaji anaweza anakazalisha kwa wingi lakini sokoni zisinunuliwe.
“Kama mnavyoona hizo zote ni chupa tupu ambazo zimekosa vinywaji na zilipaswa kuwepo sokoni na hii ni kutokana na kupandisha kodi kiholela, jambo ambalo hata Serikali haijatambua kuwa na yenyewe imekosa mapato” alisema Meneja huyo huku akionesha chupa tupu za bia.
Aliongeza kuwa serikali ilipaswa kumpandishia kodi mzalishaji na sio mlaji wa mwisho jambo ambalo linaathiri uchumi wa mtu mmoja mmoja.Alisema kwa kufanya hivyo ingekuwa rahisi kwa mzalishaji kuwa na mbinu mbadala ya kukusanya kodi kwa ajili ya kuilipa Serikali tofauti na ilivyosasa ambapo Serikali huongeza gharama ya kodi kwenye bidhaa inayopaswa kwenda sokoni.
Jemedari alisema katika kunusuru kiwanda kisifungwe uongozi wa tbl umelazimika kupunguza bei ya vinywaji tofauti na bei elekezi inayotakiwa kutokana na kiwango cha kodi ya serikali ambapo Bia moja ilipaswa kuuzwa 2500 lakini kiwanda kimepunguza hadi shilingi 2200.
Subscribe to:
Post Comments
(Atom)
TOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO

Find us on Facebook
Popular Posts
My Blog List
-
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada awasili nchini kwa ziara ya Kikazi - Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada Mhe. Randeep Sarai amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku Tatu. Mhe. Sarai anatarajiwa kutembelea miradi m...1 hour ago
-
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada awasili nchini kwa ziara ya Kikazi - Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada Mhe. Randeep Sarai amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku Tatu. Mhe. Sarai anatarajiwa kutembelea miradi m...1 hour ago
-
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada awasili nchini kwa ziara ya Kikazi - Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada Mhe. Randeep Sarai amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku Tatu. Mhe. Sarai anatarajiwa kutembelea miradi m...1 hour ago
-
Michezo : Mhandisi Hilly - Ushiriki wa watumishi katika Michezo ni chachu ya kujenga Mshikamano na Kuboresha Afya Zao - Na Oscar Assenga, TANGA USHIRIKI wa Watumishi katika michezo umetajwa kwamba ni njia nzuri ya kujenga amani na mshikamano ambao unaweza kuboresha afy...6 hours ago
-
Why are Japanese Cars so popular in the Arab World - Japanese cars have firmly established their presence in Arab markets, becoming a symbol of quality and reliability. The continued demand for these vehicl...3 days ago
-
DKT. KIKWETE: NCHI ZA AFRIKA ZINAHITAJI KUWEKEZA ZAIDI KATIKA TAFITI NA KILIMO - Na.Vero Ignatus ARUSHA Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Umasikini umefanyika Jijini Arusha kwa lengo la Kuwaunganisha wataalamu wa utafiti na watunga se...5 weeks ago
-
สมัคร wing888 VIP เว็บตรงคุณภาพสูง และบริการคุณภาพ - Wing888 vip เป็นหนึ่งในชื่อที่น่าสนใจโดยเฉพาะสำหรับผู้ที่ให้ความสำคัญกับความปลอดภัย เสถียรภาพ และระบบการให้บริการที่จริงจัง ความเป็นส่วนตัวและความซื่อสัตย...1 month ago
-
BENKI YA STANBIC YAFIKIA TAMATI KAMPENI YA TAP KIBINGWA KWA SHANGWE - • TZS milioni 7.5 zimetolewa kama zawadi kwa wateja 15 waliotumia Visa Debit Card zao kwa miezi mitatu • Washindi wengine watano wajishindia TZS 500...2 months ago
-
KIWANJA CHA NDEGE SUMBAWANGA CHAFIKIA ASILIMIA SITINI YA UJENZI. - Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga umefikia asilimia sitini ya utekelezaji wake. Taarifa hiyo imetolewa mbele waandishi wa habari leo Machi 26, 20...3 months ago
-
Majina ya Blog Zinazoanzia na Herufi ya V - *1. VOA Sauti ya America * www.voaswahili.com *2. Vijimambo* lukemusicfactory.blogspot.com4 months ago
-
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025 - Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini ke...4 months ago
-
ZANZIBAR: UBALOZI WA NORWAY TANZANIA WAIPONGEZA TAMWA-ZNZ UTEKELEZAJI MRADI WA SWIL. - *Maafisa Ubalozi wa Norway wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TAMWA-ZNZ mara baada ya kumaliza mazungumzo katika ofisi zilizopo Tu...3 years ago
-
AUDIO | Harmonize - Kushoto Kulia | Download - *DOWNLOAD* Listen to Harmonize - Kushoto Kulia byDJ Mwanga on hearthis.at5 years ago
-
-
Ufafanuzi wa TCRA kuhusu kuondoa chaneli za runinga zinazotazamwa bila kulipia (FTA) kutoka ving'amuzi vya Azam, Multichoice na Zuku - Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imefafanua kuhusu kuondoa Channel za Televisheni za ndani zinazotazamwa bila kulipia (FTA) kutoka Ving’amuzi vya Azam, Multic...6 years ago
-
MSANII ROSE MUHANDO: SIOGOPI WANAONISEMA VIBAYA - Rose Muhando. STAA wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amefunguka kuwa, haogopi watu wanaomsema kwa ubaya kila kona bali anaangalia kile kilichomsababisha ku...8 years ago
-
VIDEO: SNURA AONGELEA KUFANYA KAZI NA DON JAZZY..! - Kila mtu alilipokea kwa style yake hili suala la mtayarishaji na msanii mkubwa wa muziki barani Afrika *Don Jazzy *kujirecord video akiimba wimbo wa Chura ...8 years ago
-
PIKIPIKI YAZUA HOFU BAADA YA KUTELEKEZWA MWAKA MZIMA JIJINI DAR ES SALAAM, UKIIKARIBIA, IKIIGUSA INAJIWASHA POLISI WAGWAYA KUIPELEKA KITUONI - Mwananchi akipita kwa kuikwepa pikipiki yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika Kituo cha waendesha...8 years ago
-
-
MATUKIO MBALI MBALI YA ZIARA YA KAMPENI ZA MGOMBEA URAIS WA UKAWA KUPITIA CHADEMA KATIKA JIMBO LA HAI, MKOANI KILIMANJARO - *Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokelewa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai ...9 years ago
-
Bunge Lamkingia Kifua Zitto Kabwe......Lasema Bado ni Mbunge Halali na Spika wa Bunge ana Mamlaka Kisheria Ya Kutengua Maamuzi ya CHADEMA - Ofisi ya Bunge imesema haijapata barua yoyote kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema). Kauli ya hiyo ya Bunge im...10 years ago
-
MAPACHA 6 WALIOZALIWA MWAKA 1983 NCHINI UINGEREZA SASA NI WAKUBWA NA WAMENZA KUWA NA FAMILIA ZAO - * Bwana Na Bibi Grahan Walton wakiwa na mabinti wao sita pamoja na mjukuu wao* * Mapacha hao wa kike wakati wana miaka mitano (Kushoto kwenda kilia) Luci...10 years ago
-
New Song WAKAZI-BIGGIE - Download Here - *Wimbo mpya kutoka kwa Wakazi - Biggie* www.aloyson.com10 years ago
-
-
-
-
-
-
-
-
0 comments:
Post a Comment