Sunday, February 14, 2016
7:53 PM
| Posted by
Unknown
|
Waumini wa dini ya Kiislam wakizozana nje ya Msikiti wa Masjidi Pelapela uliopo eneo la Mtakuja Vingunguti jijini Dar es Salaam katika swala ya Ijumaa leo mchana, baada ya kutokea tafrani ya waumini hao dhidi ya viongozi wao ambao wanatuhumiwa kutafuna fedha zaidi ya sh.milioni 20 walizochanga kwa ajili ya ujenzi wa msikiti mpya.
Muumini wa Msikiti huo, Mbarouk Mohamed Makame (kushoto), akizungumza kuhusu fedha hizo zinazodaiwa kutumiwa vibaya na viongozi wao. Kulia ni mmoja wa wazee wa msikiti huo, Mzee Selasela.
Mzee Selasela akionesha dari la msikiti huo lililochakaa ambapo fedha hizo zinazodaiwa kutumiwa vibaya na viongozi wao zingesaidia kuufanyia ukarabati.

Hapa mzee Selasela akionesha uchakavu wa kapeti.
Hapa akionesha vyoo vilivyo chakaa vya msikiti huo.
Mwonekano wa vyoo vya msikiti huo vinavyotumika.
Waumini wakiwa nje ya msikiti huo wengine wakiswali.
Waumini wakiwa mbele ya vibanda vya biashara vilivyopo nje ya msikiti huo.

Watoto wa shule ya awali katika msikiti huo wakiwa na mwalimu wao (kulia)
Na Dotto Mwaibale
TAFRANI kubwa imezuka katika Msikiti wa Masjidi Pelapela uliopo eneo la Mtakuja Vingunguti jijini Dar es Salaam baada ya viongozi wa msikiti huo kudaiwa kutafuna zaidi ya sh.milioni 20.
Fedha hizo imeelezwa kuwa zilichangwa na waumini wa msikiti huo kwa ajili ya ujenzi wa msikiti mpya baada ya unaotumika kuchakaa.
Imamu mkuu wa msikiti huo aliyetajwa kwa jina la Hamidu Mitanga alilazimika kutoweka ndani ya msikiti huo baada ya kuendesha swala ya Ijumaa iliyofanyika jana mchana kutokana na waumini kuwa na jaziba kufuatia imamu huyo kutamuka kuwa hakuhitaji kuulizwa maswali yoyote kuhusu upotevu wa fedha hizo na kuwa uongozi uliopo utaendelea kuwepo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi msikitini hapo Dar es Salaam leo mchana wakati wa swala ya Ijumaa mmoja wa waumini wa msikiti huo Mbarouk Mohamed Makame alikiri kuwepo kwa ubadhilifu wa fedha za waumini zilizochangwa kwa ajili ya ujenzi wa msikiti mpya.
"Suala la upotevu wa fedha hizo lipo na limeleta changamoto kubwa kwa waumini na kusababisha kuwepo kwa makundi mawili moja likiwa lile linalolalamikiwa kutafuna fedha hizo na lile linalotaka fedha hizo zitolewe maelezo zilipo" alisema Mzee Makame.
Mzee wa msikiti huo na Mwenyekiti wa Kamati ya watu 10 Saidi Ngubi alisema fedha zinazoshindwa kutolewa maelezo ya matumizi yake na viongozi wa msikiti huo zilitokana na mradi wa maji na michango ya waumini.
"Mimi ndiye niliyeanza kuuliza matumizi ya fedha hizo lakini viongozi hao wakawa hawana majibu na badala yake waliivunja kamati yetu na kuchagua nyingine jambo lililoleta sintofahamu" alisema Ngubi.
Imamu mkuu wa msikiti huo Hamidu Mitanda alisema fedha hizo zilitumika kwa ajili ya mchakato mzima wa kupata umiliki wa kiwanja ulipo msikiti huo na michoro ya ujenzi wa msikiti mpya na kuwa yeye ndiye aliyeanzisha mpango wa kupata msikiti ulio bora na si bora msikiti.
"Binafsi sina shida na cheo hiki cha Uimamu kwani nina shughuli zangu nyingi mkitaka kuniondoa fuateni taratibu kama zili zilizoniweka madarakani na sisi kama viongozi dhamira yetu ni kuwa na msikiti uliobora wa ghorofa na si bora msikiti" alisema Mitanga.
Mitanga alisema chokochoko hizo zilianza tangu mwaka 2007 ambapo tulikubaliana kila muumini kati ya waumini 205 achangie sh.5000 za ujenzi lakini waliochangia walikuwa ni waumini wachache ambapo zilipatikana sh.milioni moja tu.
Imamu huyo alisema uongozi unaoendesha msikiti huo hauko tayari kuachia madaraka kwa tuhuma hizo ambazo hazina ukweli alizodai zinachochewa na baadhi ya waumini.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Subscribe to:
Post Comments
(Atom)
TOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO

Find us on Facebook
Popular Posts
Widget by Making Different
My Blog List
-
TANZANIA NA SWEDEN KUSHIRIKIANA KUIMARISHA MIFUMO YA UBUNIFU - NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) mkataba wa miaka mitano na Serikali ya Sweden kwa lengo la kuwezesha t...26 minutes ago
-
SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI-MAJALIWA - WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kufanya maboresho zaidi...58 minutes ago
-
MHE. NDERIANANGA ATEMBELEA MABANDA YA MAONESHO KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI - NA. MWANDISHI WETU BERLIN, UJERUMANI 03 APRILI, 2025 Matukio katika picha Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nde...1 hour ago
-
Michezo : Simba Yashindwa Kufurukuta Ugenini ,Yapigwa 2 -0 na Al Masry - KLABU ya Simba imeshindwa kutamba ugenini katika hatua ya robo fainali mkondo wa kwanza dhidi ya Al Masry ya nchini Misri baada ya kupokea kipigo cha ...16 hours ago
-
KIA Sportage R Review: Specs, Features, and Performance Breakdown - The KIA Sportage R, produced from 2010 to 2015, is a compact SUV known for its stylish design, improved ride quality, and modern features. With KIA’s sig...1 day ago
-
NELSON MANDELA NA TMA KUWAJENGEA UWEZO WATAALAMU WA HALI YA HEWA KUPITIA TEKNOLOJIA YA AKILI MNEMBA - Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali y...1 day ago
-
KIWANJA CHA NDEGE SUMBAWANGA CHAFIKIA ASILIMIA SITINI YA UJENZI. - Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga umefikia asilimia sitini ya utekelezaji wake. Taarifa hiyo imetolewa mbele waandishi wa habari leo Machi 26, 20...1 week ago
-
Majina ya Blog Zinazoanzia na Herufi ya V - *1. VOA Sauti ya America * www.voaswahili.com *2. Vijimambo* lukemusicfactory.blogspot.com4 weeks ago
-
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025 - Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini ke...4 weeks ago
-
Dog House Megaways: Slot Gacor dengan Kemenangan Besar - Pendahuluan Dog House Megaways dari Pragmatic Play adalah salah satu game slot online gacor yang populer di kalangan pemain karena fitur Megaways yang me...5 months ago
-
ZANZIBAR: UBALOZI WA NORWAY TANZANIA WAIPONGEZA TAMWA-ZNZ UTEKELEZAJI MRADI WA SWIL. - *Maafisa Ubalozi wa Norway wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TAMWA-ZNZ mara baada ya kumaliza mazungumzo katika ofisi zilizopo Tu...2 years ago
-
AUDIO | Harmonize - Kushoto Kulia | Download - *DOWNLOAD* Listen to Harmonize - Kushoto Kulia byDJ Mwanga on hearthis.at5 years ago
-
-
Ufafanuzi wa TCRA kuhusu kuondoa chaneli za runinga zinazotazamwa bila kulipia (FTA) kutoka ving'amuzi vya Azam, Multichoice na Zuku - Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imefafanua kuhusu kuondoa Channel za Televisheni za ndani zinazotazamwa bila kulipia (FTA) kutoka Ving’amuzi vya Azam, Multic...6 years ago
-
KAMPUNI YA ORYX GAS YAJIVUNIA KUWA RAFIKI WA MAZINGIRA - Na Emmanuel Masaka,Dar. KAMPUNI ya mama katika usambazaji na uuzaji wa gesi ya ORYX nchini ijulikanayo kama ORYX ENERGIES LTD imekuwa mstari wa mbe...6 years ago
-
MSANII ROSE MUHANDO: SIOGOPI WANAONISEMA VIBAYA - Rose Muhando. STAA wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amefunguka kuwa, haogopi watu wanaomsema kwa ubaya kila kona bali anaangalia kile kilichomsababisha ku...7 years ago
-
VIDEO: SNURA AONGELEA KUFANYA KAZI NA DON JAZZY..! - Kila mtu alilipokea kwa style yake hili suala la mtayarishaji na msanii mkubwa wa muziki barani Afrika *Don Jazzy *kujirecord video akiimba wimbo wa Chura ...8 years ago
-
PIKIPIKI YAZUA HOFU BAADA YA KUTELEKEZWA MWAKA MZIMA JIJINI DAR ES SALAAM, UKIIKARIBIA, IKIIGUSA INAJIWASHA POLISI WAGWAYA KUIPELEKA KITUONI - Mwananchi akipita kwa kuikwepa pikipiki yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika Kituo cha waendesha...8 years ago
-
-
MATUKIO MBALI MBALI YA ZIARA YA KAMPENI ZA MGOMBEA URAIS WA UKAWA KUPITIA CHADEMA KATIKA JIMBO LA HAI, MKOANI KILIMANJARO - *Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokelewa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai ...9 years ago
-
Bunge Lamkingia Kifua Zitto Kabwe......Lasema Bado ni Mbunge Halali na Spika wa Bunge ana Mamlaka Kisheria Ya Kutengua Maamuzi ya CHADEMA - Ofisi ya Bunge imesema haijapata barua yoyote kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema). Kauli ya hiyo ya Bunge im...10 years ago
-
MAPACHA 6 WALIOZALIWA MWAKA 1983 NCHINI UINGEREZA SASA NI WAKUBWA NA WAMENZA KUWA NA FAMILIA ZAO - * Bwana Na Bibi Grahan Walton wakiwa na mabinti wao sita pamoja na mjukuu wao* * Mapacha hao wa kike wakati wana miaka mitano (Kushoto kwenda kilia) Luci...10 years ago
-
New Song WAKAZI-BIGGIE - Download Here - *Wimbo mpya kutoka kwa Wakazi - Biggie* www.aloyson.com10 years ago
-
-
-
-
-
-
-
-
Total Pageviews
25885
0 comments:
Post a Comment