Monday, August 11, 2014


Wakati uchumi wa Tanzania ukiendelea kukua siku hadi siku, ongezeko la wananchi wenye kipato cha kati nalo limezidi kukua, na hivyo kuleta changamoto mpya katika masoko ya bidhaa mbalimbali hapa Waagizaji wa kinywaji Kutoka Uholanzi cha Bavaria eneo la Afrika ya Mashariki, Jovet (Tanzania) Limited wamedhamiria kuleta changamoto hiyo baada ya kuzindua kampeni rasmi ya mbio za kuelekea kileleni, na hivyo kuongeza wigo wake katika soko hili la Afrika ya Mashariki, ambalo limekua likikua kwa kasi kiuchumi.


Akiongea katika chakula cha jioni na mawakala wakubwa wa kinywaji hicho katika eneo la Afrika ya Mashariki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam, bwana John Kessy, Mkurugenzi mkuu wa Jovet (Tanzania) Limited, alisema, Kampeni hii ya Bavaria ya kuelekea kileleni imelenga kuleta changamoto kubwa katika eneo hili la Afrika ya mashariki, kwa kuwa litasaidia kutengeneza ajira zaidi, na kuongeza kipato binafsi na kwa serikali kwa ujumla.


Bwana Kessy aliongeza na kusema kuwa, Tumeweza kupenya katika soko hili na kutengeneza mahusiano mazuri na wafanyabiashara. Tutaendelea kukua siku hadi siku tukiwapatia wateja wetu kilicho Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia hamsini ya wanywaji wa vinywaji vya shayiri wako eneo la Mashariki ya kati na Afrika na asilimia hii hutumia hektolita milioni 18 kwa mwaka, na hii imetokana na kwamba watu wengi wamekua wakijali zaidi afya zao, na hivyo Bavaria inataka kutumia fursa hii kujikita zaidi katika eneo hili, na kuwapa fursa walaji kupata uchaguzi zaidi.


Mawakala hawa pia waliweza kupata fursa ya kujifunza mengi kuhusu kinywaji cha Bavaria, na pia mbinu za kufanya biashara katika siko hili ambalo limekua likikua kwa kasi na lenye ushindani mkubwa. Pamoja na kujifunza mengi kuhusu Bavaria na mbinu za kibiashara, mawakala hao pia waliweza kujishindia zawadi mbalimbali, zikiwemo seti za Televisheni, Simu za Mkononi na vinywaji mbalimbali vya familia ya Takwimu za hivi karibuni za mwaka 2010-2015 zinaonyesha kuwa soko la vinywaji linatarajiwa kukua na kuzalisha zaidi ya dola za kimarekani bilioni 1.9, na tafiti hii

Mkurugenzi Mkuu wa Kovet (t) limited,Ndugu John Kessy akitafakari jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni yam bio za kuelekea juu na Bavaria zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Jovet (t) Limited Ndugu John Kessy akimpongeza Bi. Christina wa K-Pub, kama mmoja wa mawakala bora wa kinywaji hicho.

Mkurugenzi wa Jovet,Ndugu John Kessy akifurahi jambo na wakala kutoka Rwanda Ndugu Innocent Gasangwa.

Baadhi mawakala wa Bavaria wakibadilishana mawazo wakati wa chakula cha jioni katika hoteli ya serana, Jijini Dar es salaam

Wakiwa kwenye picha ya pamoja,Ndugu John Kessy, Bi. Pendo Assey na mawakala kutoka Burundi, Francoise Uwizera na Innocent Gasangwa kutoka Rwanda.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

TOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO

TOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO

Find us on Facebook

Popular Posts

My Blog List

Total Pageviews

Tweets

NETWORKED BLOGS

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
widgets