Monday, August 11, 2014

Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

Staa wa muziki wa bongo fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platinum' akilitawala jukwaa pamoja na baadhi ya wacheza shoo wake katika onyesho la kwanza la tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza lililofanyika mwishoni mwa wiki,tamasha hilo litaendelea kwenye miji mingine ya Bukoba na Kahama mwishoni mwa wiki..

Baada ya kazi ya kuwaburudisha mashabiki wake,Mara Wema Sepetu a.k.a shemeji nae akajiunga kumpa sapoti mpenzi wake jukwaani

Mmoja wa wasanii anaefanya vyema kwa sasa katika anga ya muziki wa bongofleva Vanessa Mdee a.k.a V Money akitumbuiza mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza (hawapo pichani) waliojitokeza kwa wingi kushuhudia mrindimo wa tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo,tamasha hilo limefanyika mwishoni mwa wiki.

Mmoja wa wasanii anaefanya vyema kwa sasa kupitia wimbo wake mpya wa Ole Themba akiwa chini ya Kampuni mpya ya No Fake Zone,Linah Sanga akitumbuiza mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza (hawapo pichani) waliojitokeza kwa wingi kushuhudia mrindimo wa tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba lililofanyika mwishoni mwa wiki.

Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

Wasanii wa kundi la Tanikando Group kutoka Igoma, Mwanza nao wakionesha umahiri wao kupamba onesho la muziki la Serengeti fiesta 2014 lililofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa CCM Kirumba jijini humo na kuhudhuriwa na maelfu ya wapenzi na washabiki wa tamasha hilo.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

TOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO

TOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO

Find us on Facebook

Popular Posts

My Blog List

Total Pageviews

Tweets

NETWORKED BLOGS

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
widgets