Friday, March 27, 2015
11:23 AM
| Posted by
Unknown
|
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (aliyefunikwa mwamvuli) akiwasili kwenye sherehe ya siku ya wanawake duniani iliyoandaliwa na Zanzibalicious Women Group na kufanyika ndani ya ukumbi wa Salama, Bwawani Hotel mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
UTAFITI uliofanywa na taasisi ya wanawake nchini Zanzibar ya Zanzibalicious Women umeonyesha kuwa asilimia 40 ya wanawake Zanzibar, wanaishi katika mazingira duni ya umasikini kwa kutojitambua na kukosa elimu ya uelewa jinsi ya kukabiliana na mazingira waliyomo.
Akisoma risala siku ya wanawake mbele ya mgeni rasmi mke wa rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mama Mwanamwema Shein , katika siku ya wanawake hafla iliyofanyika hoteli ya Bwawani, Mweka hazina wa Zanzibalicious Women Group, Shekha Hilal alisema hali hiyo ni changamoto kubwa na sasa kunatafutwa namna ya kumfikia mwanamke huyu ambaye ameshagota katika jamii yetu.
“Mama Shein asilimia hii ni kubwa saana, na sisi kama wanawake ambao tayari tumejaaliwa elimu na tunajitambua, ikiwa ni pamoja na tayari tumepiga hatua kimaendeleo katika nyanja mbalimbali, tumeguswa sana sana na suala hili.” Alisema Shekha.
Zanzibalicious ni umoja wa wanawake wanaoishi Zanzibar,ulioanzishwa mwaka 2011,na kusajiliwa rasmi mwaka 2013, ikiambatana na uzinduzi uliofanyika tarehe 28 Machi 2014.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein akiwasili kwenye sherehe ya siku ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na Zanzibalicous Women Group mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Salama, Bwawani Hotel.
Mweka hazina huyo alisema kwamba wanajiuliza maswali mengi kama mwanamke huyo elimu ya kujikwamua imemfikia au kama kuna jitihada zozote za kumfikishia elimu hiyo.
“Je hili ni jukumu la serikali peke yake? Au sisi tunatakiwa tujumuike na serikali? mheshimiwa mgeni rasmi tumeona ya kwamba tuungane pamoja na serikali katika kutekeleza suala hili.” Alisema Shekha akielezea nia ya taasisi hiyo ya kuondoa umaskini miongoni mwa wanawake nchini Zanzibar.
Alisema taasisi yao inajipanga kutoa elimu za aina mbili ili awali kumuwezesha kujikimu kupitia ujasiriamali, kwa kumpatia elimu kwa vitendo,kwa mfano:-ushonaji,ufugaji na utengenezaji wa bidhaa mbali mbali na pili kumtoa katika hali ya upweke ili elimu atakayopata imfikishe kwenye mifuko mbali mbali pamoja na mfuko wa Rais Dk. Ali Mohammed Shein .
Alisema katika program hiyo wanatarajia baada ya miaka 2 wanawake 100 watakuwa wanajitegemea wenyewe na kuwa mabalozi katika kuelimisha wanawake wengine zaidi.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein akisoma hotuba wakati wa sherehe ya siku ya wanawake duniani iliyoandaliwa na Zanzibalicous Women Group na kufanyika ndani ukumbi wa Salama, Bwawani hoteli mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akifuatiwa na Mwenyekiti mstaafu wa Zanzibalicious Women Group, Bi. Ummukulthum Ansel.
“Na kama kila mwanamke akiweza kuelimisha wanawake katika kaya yake ,baada ya miaka kadhaa, Zanzibar itakuwa na wanawake walioweza kujikomboa katika dimbwi hili la kuishi maisha duni.” Alisema.
Akizungumzia mafanikio ya asasi hiyo alisema kwamba imefanikiwa kutoa elimu na kuwawezesha kina mama kuunda vikundi vidogo vidogo vya maendeleo kwa kuanzisha miradi mbalimbali, kwa mfano kina mama wa Chaani na Matemwe.
Aidha imetoa misaada ya hali na mali kwa waathirika wa madawa ya kulevya ikiwa ni moja ya kumkwamua mwanamke na kutoa misaada mbali mbali kwa wanawake wasiojiweza ikiwemo hospital kuu ya Mnazi mmoja na kina mama wajane.
Alisema pamoja na mafanikio hayo bado wanawake wanakabiliwa na changamoto za ndoa za utotoni, uzazi salama, ukatili wa kijinsia,mfumo dume, ubaguzi na mimba za utotoni.
Mhe.Mgeni rasmi, Umoja huu umekuwa ukiendesha shughuli zote tokea mwaka 2011 kwa kutegemea michango yetu sisi binafsi.
Baadhi ya wakinama waliohudhuria sherehe hiyo wakionekana kufurahishwa na hotuba ya Mke wa Rais wa Zanzibar (hayupo pichani).
Changamoto hii imesababisha kutokutimiza kwa malengo yetu kwa muda tulioupanga kutokana na kukosa fedha za kutosheleza utekelezaji wa malengo hayo.
Akijibu risala hiyo Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein, ameikumbusha jamii kuunganisha nguvu zao kuwakomboa wanawake kujiendeleza kimaisha na kujiongezea kipato.
Alisema hatua hiyo itaongeza kasi ya kuimarisha ustawi wa familia na jamii hususan wanawake wanaoishi vijijini ambao wanakabiliwa na changamoto zaidi.
Alisema sherehe ya siku ya wanawake duniani inakuwa na maana zaidi kama juhudi zitafanyika kuangalia changamoto na kujipanga kuzifanyia kazi.
“Rai yangu ni kuwa tuwazingatie zaidi akina mama wanaoishi vijijini na wenye mahitaji maalum kutokana na kukosa fursa kama hizo za kuwaendeleza kimaisha”, alisisitiza.
Mweka hazina wa Zanzibalicious Women Group, Bi. Shekha Hilal akisoma risala kwa mgeni rasmi Mke wa Rais wa Zanzibar (hayupo pichani) Kulia ni Mwenyekiti wa Zanzibalicous Women Group, Bi. Evelyne Wilson.
Aidha, aliongeza kuwa wanawake ni jeshi kubwa ambalo likiandaliwa vyema linaweza kushinda katika mapambano yanayokusudiwa huku akisisitza mshikamano ili kufikia malengo yanayowekwa.
Akizungumzia ujumbe wa sherehe hizo ambao ni kuhamasisha hatua mathubuti kumwendeleza na kumtambua mwanamke, alitoa rai kwa wanawake kushirikiana na serikali katika kampeni za kupambana na madhila wanayokabiliana nayo ikiwa ni pamoja na ukatili wa watoto na wanawake.
Kuhusu uzoefu wake katika maisha na malezi ya watoto, alisema amebahatika kupata watoto 11 ambao amewalea katika mazingira mbalimbali ikiwa ni kwenda na kurudi kazini na kuwa pekee huku mumewe akiwa safarini kikazi.
Aidha, aliwataka wanawake kuwa wastahamilivu katika malezi ya watoto hasa watoto Njiti ambao huzaliwa kabla ya kufikisha muda.
Hata hivyo aliwaonya wanawake wanaojali kujiremba na kuwa sahau watoto na kukumbusha kwa ‘watoto ni wageni’ kwamba wanahitaji matunzo na ukarimu mkubwa kutoka kwa wazazi wao.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizindua Mfuko wa Zanzibalicious Women Group kwa kuchangia shilingi milioni tano, wakati wa maadhimisho ya sherehe ya wanawake duniani visiwani Zanzibar yaliyoandaliwa na Zanzibalicious Women Group na kufanyika katika ukumbi wa Salama uliopo Bwawani Hotel Zanzibar. Kulia ni Mwenyekiti wa Zanzibalicious Women Group, Bi Evelyne Wilson Baruti.
Mweka hazina wa Zanzibalicious Women Group, Shekha Hilal akinakili majina ya watu waliokuwa wakichangia kwenye harambe ya mfuko wa Zanzibalicous Women Group uliozinduliwa rasmi na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (hayupo pichani).
Mbunifu nguli wa mavazi Mama wa mitindo, Asia Idarous akinadi moja ya nguo alizotengeneza kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Zanzibalicious Women Group.
Mke wa Naibu Waziri wa Afya serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Zakhia Kombo akitangaza dau la kununua nguo hiyo iliyokuwa ikinadiwa kwenye harambe ya mfuko wa ZWG iliyozinduliwa na Mama Mwanamwema Shein.
Meza kuu kwenye picha ya pamoja na Zanzibalicous Women Group.
Unaweza kutembelea mtandao wao na kuona shughuli mbalimbali walizozifanya hapa http://www.zanzibalicious.org/
Mmoja wa wadhamini ZANLINK wanaotoa udhamini kwa Zanzibalicious Women Group wakisikiliza kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbini hapo. Kwa picha zaidi bofya link hii
Subscribe to:
Post Comments
(Atom)
TOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO

Find us on Facebook
Popular Posts
UFISADI WA SHILINGI MILIONI 20 WAZUA TAFRANI MSIKITINI JIJINI DAR ES SALAAM
14 Feb 2016 AnonymousBE FORWARD SUPPORTERS
14 Feb 2016 AnonymousBE FORWARD SUPPORTERS
14 Feb 2016 AnonymousShilling hits record lows on higher dollar demand
21 Apr 2015 AnonymousNew bridge upgrades Kigamboni
21 Apr 2015 AnonymousTNBC urges increased investment in education
21 Apr 2015 AnonymousMdee, nine others case hearing set for May 4
21 Apr 2015 AnonymousTEA accomplishes 39bn/- projects
21 Apr 2015 AnonymousCentre offers 250 acres for public servants’ houses
21 Apr 2015 AnonymousCall for early disaster warning system in ocean
21 Apr 2015 AnonymousUnappreciative onion traders irk Singida RC
21 Apr 2015 AnonymousTanzanians safe in South Africa
21 Apr 2015 AnonymousMilitants Kill 147 In Kenyan University Attack
03 Apr 2015 AnonymousMAPIGANO KATI YA JESHI NA AL SHABAAB BADO YANAENDELEA KATIKA CHUO KIKUU CHA GARRISSA AMBAPO WANAFUNZI 15 WAMEUAWA
03 Apr 2015 AnonymousBREAKING NEWS-TUME YA UCHAGUZI NEC YAARISHA KURA YA MAONI
03 Apr 2015 AnonymousAUWA NDUGUZE NA KUWALA KWA CHUMVI
03 Apr 2015 AnonymousKenya attack: Garissa University assault 'killed 147'
03 Apr 2015 AnonymousGovt now drops move to rush information bill
28 Mar 2015 AnonymousUN set to investigate albino killings in EA
28 Mar 2015 AnonymousHow Nigeria's presidential election works
28 Mar 2015 AnonymousGerman pilot 'hid evidence of illness' from employers
28 Mar 2015 AnonymousSomali official says siege on Mogadishu hotel over
28 Mar 2015 AnonymousYemen crisis tops agenda as Arab League summit opens
28 Mar 2015 AnonymousLISSU AWAKATAZA WABUNGE WA CHADEMA KWENDA KWENYE UZINDUZI WA ACT
28 Mar 2015 AnonymousKAULI YA ZITTO KABWE KUHUSU UONGOZI WA CHAMA CHA ACT
28 Mar 2015 AnonymousMAAJABU YA MWAKA..MEYA JERRY SILAA AHAMISHIA OFISI MTAANI HUKO UKONGA.
28 Mar 2015 AnonymousBONDIA MOHAMED MATUMLA ALIVYOMCHAKAZA MCHINA USIKU WA JANA
28 Mar 2015 AnonymousPSPF WAFANYA KIKAO KAZI NA WATUMISHI WA MANISPAA, DAR NA PWANI
27 Mar 2015 AnonymousNI MAOMBOLEZO NA VILIO UJERUMANI NA HISPANIA
27 Mar 2015 AnonymousBunge lapitisha muswada, sasa waandishi kufungwa jela ikiwa..........
27 Mar 2015 Anonymous
Widget by Making Different
My Blog List
-
Habari : THRDC yatoa Jacketi za usalama kwa JOWUTA - .Yamuomba Rais Maridhiano ya Kisiasa Na. Vero Ignatus ,Dar es Saalam. MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania(THRDC) umekabidhi jaketi za usa...8 hours ago
-
RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KULETA SERIKALI KWA WANANCHI ILI KULETA MAENDELEO - MHE. MCHENGERWA - Na John Mapepele Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Sulu...9 hours ago
-
RWEBANGIRA AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA ZAO KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena K.Rwebangira ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya kujitokea na kufika kwenye vituo vya kujiand...10 hours ago
-
RWEBANGIRA AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA ZAO KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena K.Rwebangira ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya kujitokea na kufika kwenye vituo vya kujiand...10 hours ago
-
RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KULETA SERIKALI KWA WANANCHI ILI KULETA MAENDELEO - MHE. MCHENGERWA - Na John Mapepele Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluh...10 hours ago
-
BEFORWARD Free Car Giveaway (SABASABA EVENT 2025) - Stand a chance to win the prizes! BE FORWARD is running a Giveaway Campaign just for Tanzania!We’re giving away 3 incredible cars to show our appreciatio...3 days ago
-
BENKI YA STANBIC YAFIKIA TAMATI KAMPENI YA TAP KIBINGWA KWA SHANGWE - • TZS milioni 7.5 zimetolewa kama zawadi kwa wateja 15 waliotumia Visa Debit Card zao kwa miezi mitatu • Washindi wengine watano wajishindia TZS 500...1 week ago
-
KIWANJA CHA NDEGE SUMBAWANGA CHAFIKIA ASILIMIA SITINI YA UJENZI. - Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga umefikia asilimia sitini ya utekelezaji wake. Taarifa hiyo imetolewa mbele waandishi wa habari leo Machi 26, 20...5 weeks ago
-
Majina ya Blog Zinazoanzia na Herufi ya V - *1. VOA Sauti ya America * www.voaswahili.com *2. Vijimambo* lukemusicfactory.blogspot.com1 month ago
-
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025 - Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini ke...2 months ago
-
Dog House Megaways: Slot Gacor dengan Kemenangan Besar - Pendahuluan Dog House Megaways dari Pragmatic Play adalah salah satu game slot online gacor yang populer di kalangan pemain karena fitur Megaways yang me...6 months ago
-
ZANZIBAR: UBALOZI WA NORWAY TANZANIA WAIPONGEZA TAMWA-ZNZ UTEKELEZAJI MRADI WA SWIL. - *Maafisa Ubalozi wa Norway wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TAMWA-ZNZ mara baada ya kumaliza mazungumzo katika ofisi zilizopo Tu...2 years ago
-
AUDIO | Harmonize - Kushoto Kulia | Download - *DOWNLOAD* Listen to Harmonize - Kushoto Kulia byDJ Mwanga on hearthis.at5 years ago
-
-
Ufafanuzi wa TCRA kuhusu kuondoa chaneli za runinga zinazotazamwa bila kulipia (FTA) kutoka ving'amuzi vya Azam, Multichoice na Zuku - Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imefafanua kuhusu kuondoa Channel za Televisheni za ndani zinazotazamwa bila kulipia (FTA) kutoka Ving’amuzi vya Azam, Multic...6 years ago
-
MSANII ROSE MUHANDO: SIOGOPI WANAONISEMA VIBAYA - Rose Muhando. STAA wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amefunguka kuwa, haogopi watu wanaomsema kwa ubaya kila kona bali anaangalia kile kilichomsababisha ku...7 years ago
-
VIDEO: SNURA AONGELEA KUFANYA KAZI NA DON JAZZY..! - Kila mtu alilipokea kwa style yake hili suala la mtayarishaji na msanii mkubwa wa muziki barani Afrika *Don Jazzy *kujirecord video akiimba wimbo wa Chura ...8 years ago
-
PIKIPIKI YAZUA HOFU BAADA YA KUTELEKEZWA MWAKA MZIMA JIJINI DAR ES SALAAM, UKIIKARIBIA, IKIIGUSA INAJIWASHA POLISI WAGWAYA KUIPELEKA KITUONI - Mwananchi akipita kwa kuikwepa pikipiki yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika Kituo cha waendesha...8 years ago
-
-
MATUKIO MBALI MBALI YA ZIARA YA KAMPENI ZA MGOMBEA URAIS WA UKAWA KUPITIA CHADEMA KATIKA JIMBO LA HAI, MKOANI KILIMANJARO - *Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokelewa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai ...9 years ago
-
Bunge Lamkingia Kifua Zitto Kabwe......Lasema Bado ni Mbunge Halali na Spika wa Bunge ana Mamlaka Kisheria Ya Kutengua Maamuzi ya CHADEMA - Ofisi ya Bunge imesema haijapata barua yoyote kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema). Kauli ya hiyo ya Bunge im...10 years ago
-
MAPACHA 6 WALIOZALIWA MWAKA 1983 NCHINI UINGEREZA SASA NI WAKUBWA NA WAMENZA KUWA NA FAMILIA ZAO - * Bwana Na Bibi Grahan Walton wakiwa na mabinti wao sita pamoja na mjukuu wao* * Mapacha hao wa kike wakati wana miaka mitano (Kushoto kwenda kilia) Luci...10 years ago
-
New Song WAKAZI-BIGGIE - Download Here - *Wimbo mpya kutoka kwa Wakazi - Biggie* www.aloyson.com10 years ago
-
-
-
-
-
-
-
-
Total Pageviews
26247
0 comments:
Post a Comment