Friday, March 27, 2015
2:29 PM
| Posted by
Unknown
|

Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali akichangia mjadala katika kikao cha Bunge, mjini Dodoma. Picha na Anthony Siame
Dodoma. Mvutano mkali uliibuka jana bungeni wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha Muswada wa Takwimu wa mwaka 2013, baada ya wabunge kuupinga. Muswada huo una kipengele kinachotoa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini isiyopungua Sh10 milioni kwa mtu au chombo cha habari kitakachofanya makosa ya kutoa takwimu zisizokuwa sahihi.
Wabunge hao waliufananisha muswada huo na miswada miwili ya habari ya mwaka 2015 ambayo itawasilishwa bungeni Jumanne chini ya hati ya
dharura kwa usiri uliopo na mpango wa kuiwasilisha bila wadau kushirikishwa.
Awali, muswada wa Takwimu uliwasilishwa kwenye mkutano wa 17 wa Bunge uliofanyika Novemba mwaka jana na wabunge wakapinga vifungu vinavyobana waandishi wa habari kuhusu eneo la takwimu, ndipo Serikali ilipoamua kuutoa kwa maelezo kuwa inakwenda kuurekebisha hadi ilipourejesha jana na ukapitishwa kwa mbinde.
Jana, Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha muswada huo, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alihoji juu ya kifungu hicho kinachotoa adhabu kali na Serikali kujibu kuwa imeshakifanyia marekebisho.
Hata hivyo, Mnyika hakukubaliana na maelezo hayo, bali alisema kifungu hicho hakijafanyiwa marekebisho yoyote na Serikali na adhabu bado inaendelea kuwa kali.
Mnyika aliungwa mkono na mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya aliyehoji, “Iweje Serikali iweke kinga kwa mtumishi wa Serikali anayetoa taarifa zisizo sahihi lakini ikaacha kuweka kwa mwandishi anayepewa taarifa hizo zisizo sahihi na ofisa huyo wa Serikali?”
Maelezo ya Bulaya yalimfanya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju kusimama na kusema kwa kifupi kuwa “mwandishi atakwenda kujieleza mahakamani au polisi.”
Ilivyokuwa mwaka jana
Kabla ya kuondolewa bungeni Novemba 2014 muswada huo pamoja na mambo mengine, ulikuwa ukipendekeza faini ya Sh10 milioni au kifungo cha mwaka mmoja jela au vyote kwa chombo cha habari kitakachotoa taarifa za kitakwimu za uongo au zenye upotoshaji.
“Mtu yeyote, kwa kujifanya anatimiza majukumu yake, iwapo anapata au anaomba kupatiwa taarifa ambayo haijaidhinishwa kuipata na kuichapisha au kuisambaza atakuwa amefanya kosa ambalo adhabu yake ni kifungo kisichopungua miezi 12 au faini isiyopungua shilingi milioni mbili au vyote kwa pamoja,” ilisema ibara ya 37 (d) cha muswada huo.
Muswada huo pia ulikuwa ukiainisha kwamba takwimu rasmi ni zile ambazo zimetolewa na kuidhinishwa na taasisi zilizoelezwa kwenye ibara hiyo ya 20 na ndizo pekee zinazoweza kutumika kama ushahidi kwenye kesi.
Adhabu kali pia zimependekezwa kwenye muswada huo kwa vyombo vya habari ambavyo vitatoa taarifa za takwimu zitakazosababisha watu wasishiriki kwenye shughuli zilizoandaliwa na Serikali zinazohusiana na masuala ya takwimu.CHANZO MWANAINCHI
Subscribe to:
Post Comments
(Atom)
TOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO
Find us on Facebook
Popular Posts
My Blog List
-
SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO LAANZA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO 2026-2031 - Shirika la Masoko ya Kariakoo limeanza rasmi maandalizi ya Mpango Mkakati mpya wa miaka mitano 2026-2031, hatua inayolenga kulifanya soko hilo la kimataifa...3 hours ago
-
SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO LAANZA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO 2026-2031 - Shirika la Masoko ya Kariakoo limeanza rasmi maandalizi ya Mpango Mkakati mpya wa miaka mitano 2026-2031, hatua inayolenga kulifanya soko hilo la kimataifa...3 hours ago
-
BODI YA USIMAMIZI WA STAKABADHI ZA GHALA YAZINDULIWA DODOMA - NAIBU Waziri wa Kilimo. Mhe. David Silinde (Mb) amesema Wizara ya Kilimo inaamini katika Mfumo wa Stakabadhi Ghalani, na kuhakikisha mfumo huo unaleta...5 hours ago
-
Tuzo : Rais Mwinyi Apokea Tuzo - Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa wito kwa taasisi na wadau wa sekta ya utalii kuongeza ushiri...11 hours ago
-
2025 Toyota Land Cruiser 70-Series Review: Price, Specs, Engine Power, Off-Road Performance & Interior Upgrades - Introduction The 2025 Toyota Land Cruiser 70-Series is back, tougher, smarter, and more capable than ever. This iconic off-road SUV blends legendary Toyo...2 weeks ago
-
UNESCO Yaunga Mkono Juhudi za Serikali Kuboresha Mfumo wa Usimamizi wa Mafunzo Endelevu ya Walimu (MEWAKA) - [image: Picture1] [image: Picture2] [image: Picture3] [image: Picture4] [image: Picture5] Na Mwandishi Wetu, Arusha. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknol...3 months ago
-
สมัคร wing888 VIP เว็บตรงคุณภาพสูง และบริการคุณภาพ - Wing888 vip เป็นหนึ่งในชื่อที่น่าสนใจโดยเฉพาะสำหรับผู้ที่ให้ความสำคัญกับความปลอดภัย เสถียรภาพ และระบบการให้บริการที่จริงจัง ความเป็นส่วนตัวและความซื่อสัตย...6 months ago
-
BENKI YA STANBIC YAFIKIA TAMATI KAMPENI YA TAP KIBINGWA KWA SHANGWE - • TZS milioni 7.5 zimetolewa kama zawadi kwa wateja 15 waliotumia Visa Debit Card zao kwa miezi mitatu • Washindi wengine watano wajishindia TZS 500...7 months ago
-
KIWANJA CHA NDEGE SUMBAWANGA CHAFIKIA ASILIMIA SITINI YA UJENZI. - Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga umefikia asilimia sitini ya utekelezaji wake. Taarifa hiyo imetolewa mbele waandishi wa habari leo Machi 26, 20...8 months ago
-
Majina ya Blog Zinazoanzia na Herufi ya V - *1. VOA Sauti ya America * www.voaswahili.com *2. Vijimambo* lukemusicfactory.blogspot.com9 months ago
-
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025 - Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini ke...9 months ago
-
ZANZIBAR: UBALOZI WA NORWAY TANZANIA WAIPONGEZA TAMWA-ZNZ UTEKELEZAJI MRADI WA SWIL. - *Maafisa Ubalozi wa Norway wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TAMWA-ZNZ mara baada ya kumaliza mazungumzo katika ofisi zilizopo Tu...3 years ago
-
AUDIO | Harmonize - Kushoto Kulia | Download - *DOWNLOAD* Listen to Harmonize - Kushoto Kulia byDJ Mwanga on hearthis.at6 years ago
-
-
Ufafanuzi wa TCRA kuhusu kuondoa chaneli za runinga zinazotazamwa bila kulipia (FTA) kutoka ving'amuzi vya Azam, Multichoice na Zuku - Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imefafanua kuhusu kuondoa Channel za Televisheni za ndani zinazotazamwa bila kulipia (FTA) kutoka Ving’amuzi vya Azam, Multic...7 years ago
-
MSANII ROSE MUHANDO: SIOGOPI WANAONISEMA VIBAYA - Rose Muhando. STAA wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amefunguka kuwa, haogopi watu wanaomsema kwa ubaya kila kona bali anaangalia kile kilichomsababisha ku...8 years ago
-
VIDEO: SNURA AONGELEA KUFANYA KAZI NA DON JAZZY..! - Kila mtu alilipokea kwa style yake hili suala la mtayarishaji na msanii mkubwa wa muziki barani Afrika *Don Jazzy *kujirecord video akiimba wimbo wa Chura ...8 years ago
-
PIKIPIKI YAZUA HOFU BAADA YA KUTELEKEZWA MWAKA MZIMA JIJINI DAR ES SALAAM, UKIIKARIBIA, IKIIGUSA INAJIWASHA POLISI WAGWAYA KUIPELEKA KITUONI - Mwananchi akipita kwa kuikwepa pikipiki yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika Kituo cha waendesha...9 years ago
-
-
MATUKIO MBALI MBALI YA ZIARA YA KAMPENI ZA MGOMBEA URAIS WA UKAWA KUPITIA CHADEMA KATIKA JIMBO LA HAI, MKOANI KILIMANJARO - *Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokelewa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai ...10 years ago
-
Bunge Lamkingia Kifua Zitto Kabwe......Lasema Bado ni Mbunge Halali na Spika wa Bunge ana Mamlaka Kisheria Ya Kutengua Maamuzi ya CHADEMA - Ofisi ya Bunge imesema haijapata barua yoyote kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema). Kauli ya hiyo ya Bunge im...10 years ago
-
MAPACHA 6 WALIOZALIWA MWAKA 1983 NCHINI UINGEREZA SASA NI WAKUBWA NA WAMENZA KUWA NA FAMILIA ZAO - * Bwana Na Bibi Grahan Walton wakiwa na mabinti wao sita pamoja na mjukuu wao* * Mapacha hao wa kike wakati wana miaka mitano (Kushoto kwenda kilia) Luci...10 years ago
-
New Song WAKAZI-BIGGIE - Download Here - *Wimbo mpya kutoka kwa Wakazi - Biggie* www.aloyson.com10 years ago
-
-
-
-
-
-
-
-

0 comments:
Post a Comment