Friday, March 13, 2015
10:17 PM
| Posted by
Unknown
|

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe Benson Mpesya juu ya madhara makubwa ya mali na maisha ya watu wakati wa ziara maalum ya kutoa pole kwa wahanga wa mvua iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.





Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa familia zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya makazi ya dharura kwa familia zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapa mkono wa pole waalimu wa shule ya msingi ya Mwakata, wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, ambao pia ni waathirika wa mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mamia ya wananchi baada ya kutembelea na kuzifariji familia zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Machi 12, 2015, amefanya ziara maalum ya kutoa pole kwa wahanga wa mvua iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Rais Kikwete amewasili mjini Kahama kiasi cha saa nane mchana baada ya ndege yake kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Mgodi wa Buzwagi na kwa muda wa kiasi cha saa tatu ametembelea familia ambazo zimepata madhara makubwa zaidi kutokana na mvua hiyo iliyonyesha kwa kiasi cha saa moja tu kuanzia saa nne usiku Machi 3, mwaka huu, 2015 na kuambana na upepo mkali na mawe.
Watu 47 walipoteza maisha, 112 wakaumia, nyumba 657 zikabomolewa ama kuharibiwa na kaya 468 kuathirika katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata na tokea siku ya maafa, Serikali imetoa huduma za dharura za chakula, sehemu za kulala, huduma za afya na huduma nyingine muhimu kwa binadamu.
Baada ya kupatiwa maelezo ya kina na uongozi wa Mkoa wa Shinyanga chini ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Ali N. Lufunga, Rais Kikwete ameanzia ziara yake katika Kijiji cha Maghuhumwa, nyumbani kwa Bwana Masemba Maburi, ambaye alipoteza watoto watano katika maafa hayo. Rais Kikwete ametoa pole kwa wafiwa na kuzungumza na wananchi waliokuwepo kwenye msiba.
Bwana Maburi ambaye sasa anaishi katika nyumba ya jirani pamoja na familia yake na familia nyingine tatu amemweleza Rais Kikwete jinsi nyumba mbili ambako watoto hao na mama yao walipokuwa wamelala zilivyoanguka na mama huyo akalazimika kukimbilia nje kwa nia ya kutafuta msaada lakini watoto wakazidiwa na kupoteza maisha.
“Sijawahi kuona mvua kubwa, kali na yenye upepo mkali kiasi kile katika maisha yangu. Mvua ilianza saa nne usiku na ikanyesha kwa muda mfupi sana, nyumba zikaanguka ama kubomolewa. Jameni tusaidie kwa sababu tumekwazika,”Bwana Maburi amemwambia Rais Kikwete.
Baada ya kutoka katika Kijiji cha Maghuhumwa, Rais Kikwete amekwenda katika Kijiji cha Nhumbi ambako amempa pole Bwana Zacharia Limbe na familia yake ambayo ilipoteza wajukuu wanne katika maafa hayo ya mwanzoni mwa mwezi huu.
Akiwa nyumbani kwa Bwana Limbe, Rais Kikwete ametembea na kujionea makazi mapya ya dharura ya familia ambayo yamejengwa kwa msaada wa Serikali.
Baada ya kuondoka kwa Bwana Limbe, Rais Kikwete ametembelea eneo la makazi ya walimu wa Shule ya Msingi ya Mwakata, ambako walimu hao wamehifadhiwa katika fremu za maduka kutokana na athari za maafa hayo. Rais Kikwete amewapa pole walimu hao na kuwaambia: “Pole sana. Tuko pamoja.
Tutaendelea kusaidiana kuona jinsi gani mnavyoweza kurejea katika maeneo yenu ya makazi ya kawaida.”
Rais Kikwete ataondoka kesho, Ijumaa, Machi 13, 2015, kurejea Dar es Salaam baada ya ziara hiyo maalum ya siku mbili katika Mkoa wa Shinyanga.
Subscribe to:
Post Comments
(Atom)
TOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO

Find us on Facebook
Popular Posts
My Blog List
-
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI BELARUS - - Kukutana na Waziri Mkuu Alexander Turchin Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Julai 21, 2025 amewasili nchini Belarus kuanza ziara ya kikazi nchini humo. Kwenye...38 minutes ago
-
NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA AZURU NACTVET - Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia Elimu, Dkt. Hussein Omar akizungumza na Katibu Mtendaji wa NACTVET, Dkt. Mwa...1 hour ago
-
NBC Yakutana na Wateja Wake Wakubwa wa Jijini Arusha, Yajadili Fursa, Ufanisi wa Huduma Zake Kwa wateja. - Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekutana na wateja wake wakubwa kutoka kampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) wa jijini Arusha ili k...9 hours ago
-
Biashara : NBC Yakutana na Wateja Wake Wakubwa wa Jijini Arusha - Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekutana na wateja wake wakubwa kutoka kampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) wa jijini Arusha il...9 hours ago
-
Bashiri Kumpata Bingwa wa EPL 2025/26 - HUKU zikiwa zimebaki wiki chache Ligi kuu ya Uingereza irejee, timu mbalimbali zinaendelea kufanya usajili kujiweka sawa kwenye msimu unaofuata wa 202...1 day ago
-
Why are Japanese Cars so popular in the Arab World - Japanese cars have firmly established their presence in Arab markets, becoming a symbol of quality and reliability. The continued demand for these vehicl...4 days ago
-
สมัคร wing888 VIP เว็บตรงคุณภาพสูง และบริการคุณภาพ - Wing888 vip เป็นหนึ่งในชื่อที่น่าสนใจโดยเฉพาะสำหรับผู้ที่ให้ความสำคัญกับความปลอดภัย เสถียรภาพ และระบบการให้บริการที่จริงจัง ความเป็นส่วนตัวและความซื่อสัตย...2 months ago
-
BENKI YA STANBIC YAFIKIA TAMATI KAMPENI YA TAP KIBINGWA KWA SHANGWE - • TZS milioni 7.5 zimetolewa kama zawadi kwa wateja 15 waliotumia Visa Debit Card zao kwa miezi mitatu • Washindi wengine watano wajishindia TZS 500...3 months ago
-
KIWANJA CHA NDEGE SUMBAWANGA CHAFIKIA ASILIMIA SITINI YA UJENZI. - Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga umefikia asilimia sitini ya utekelezaji wake. Taarifa hiyo imetolewa mbele waandishi wa habari leo Machi 26, 20...3 months ago
-
Majina ya Blog Zinazoanzia na Herufi ya V - *1. VOA Sauti ya America * www.voaswahili.com *2. Vijimambo* lukemusicfactory.blogspot.com4 months ago
-
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025 - Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini ke...4 months ago
-
ZANZIBAR: UBALOZI WA NORWAY TANZANIA WAIPONGEZA TAMWA-ZNZ UTEKELEZAJI MRADI WA SWIL. - *Maafisa Ubalozi wa Norway wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TAMWA-ZNZ mara baada ya kumaliza mazungumzo katika ofisi zilizopo Tu...3 years ago
-
AUDIO | Harmonize - Kushoto Kulia | Download - *DOWNLOAD* Listen to Harmonize - Kushoto Kulia byDJ Mwanga on hearthis.at5 years ago
-
-
Ufafanuzi wa TCRA kuhusu kuondoa chaneli za runinga zinazotazamwa bila kulipia (FTA) kutoka ving'amuzi vya Azam, Multichoice na Zuku - Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imefafanua kuhusu kuondoa Channel za Televisheni za ndani zinazotazamwa bila kulipia (FTA) kutoka Ving’amuzi vya Azam, Multic...6 years ago
-
MSANII ROSE MUHANDO: SIOGOPI WANAONISEMA VIBAYA - Rose Muhando. STAA wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amefunguka kuwa, haogopi watu wanaomsema kwa ubaya kila kona bali anaangalia kile kilichomsababisha ku...8 years ago
-
VIDEO: SNURA AONGELEA KUFANYA KAZI NA DON JAZZY..! - Kila mtu alilipokea kwa style yake hili suala la mtayarishaji na msanii mkubwa wa muziki barani Afrika *Don Jazzy *kujirecord video akiimba wimbo wa Chura ...8 years ago
-
PIKIPIKI YAZUA HOFU BAADA YA KUTELEKEZWA MWAKA MZIMA JIJINI DAR ES SALAAM, UKIIKARIBIA, IKIIGUSA INAJIWASHA POLISI WAGWAYA KUIPELEKA KITUONI - Mwananchi akipita kwa kuikwepa pikipiki yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika Kituo cha waendesha...8 years ago
-
-
MATUKIO MBALI MBALI YA ZIARA YA KAMPENI ZA MGOMBEA URAIS WA UKAWA KUPITIA CHADEMA KATIKA JIMBO LA HAI, MKOANI KILIMANJARO - *Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokelewa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai ...9 years ago
-
Bunge Lamkingia Kifua Zitto Kabwe......Lasema Bado ni Mbunge Halali na Spika wa Bunge ana Mamlaka Kisheria Ya Kutengua Maamuzi ya CHADEMA - Ofisi ya Bunge imesema haijapata barua yoyote kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema). Kauli ya hiyo ya Bunge im...10 years ago
-
MAPACHA 6 WALIOZALIWA MWAKA 1983 NCHINI UINGEREZA SASA NI WAKUBWA NA WAMENZA KUWA NA FAMILIA ZAO - * Bwana Na Bibi Grahan Walton wakiwa na mabinti wao sita pamoja na mjukuu wao* * Mapacha hao wa kike wakati wana miaka mitano (Kushoto kwenda kilia) Luci...10 years ago
-
New Song WAKAZI-BIGGIE - Download Here - *Wimbo mpya kutoka kwa Wakazi - Biggie* www.aloyson.com10 years ago
-
-
-
-
-
-
-
-
0 comments:
Post a Comment