Friday, March 13, 2015
10:05 PM
| Posted by
Unknown
|
Stori: Mwandishi wetu
SIKU za masikitiko bado zinaendelea kwa waziri mkuu aliyejizulu, Edward Lowassa baada ya kuwepo kwa taarifa za kukesha akilia, kisa kikitajwa kuwa ni mwendelezo ya maombolezo ya kifo cha Mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM), Kapteni John Komba.Kapteni Komba alifariki dunia Februari 28, mwaka huu jijini Dar na kuzikwa kijijini kwao, Lituhi mkoani Ruvuma, Machi 3.
Waziri mkuu aliyejizulu, Edward Lowassa.Chanzo cha habari cha kuaminika kutoka kwa Lowassa kimefichua kuwa msiba huo ungali unamtesa waziri mkuu huyo wa zamani kiasi cha kububujikwa na machozi kila mara na hasa nyakati za usiku.
KIPI KINAMLIZA LOWASSA?
“Mfano juzi (Jumatatu, Machi 9) naambiwa hakulala, alikesha analia, inaonekana alimpenda kwa dhati (Komba), pengine ni kwa sababu alijitoa kumtetea, kumpigania na kumfariji kwenye mapambano yake ya kisiasa, tangu msiba huo utokee amekuwa kwenye wakati mgumu, siyo yeye peke yake hata mkewe (Regina Lowassa), wote wamefadhaika,” kilisema chanzo.
Uwazi Mizengwe lilipokidadisi chanzo hicho kwa nini mheshimiwa huyo awe na wakati mgumu zaidi usiku, maelezo yalikuwa ni kwamba, huo ndiyo wakati ambao Lowassa hupata muda wa kupumzika na kutafakari maisha yake.
“Anapopata utulivu humkumbuka, mmoja kati ya watoto wake aliniambia kuwa kauli za mzee wao mara kwa mara ni kuona wanahuzunika naye pamoja ili hata wakipata fursa ya kufurahi, wafurahi pamoja naye.
“Nafikiri unakumbuka Kapteni Komba alitangaza hadharani kuwa anamuunga mkono Lowassa na yuko tayari hata kufukuzwa chama, nadhani akikumbuka upiganaji wake na kuona amefariki dunia anashindwa kuzuia huzuni, matokeo yake anabubujikwa machozi,” kilisema chanzo hicho.
LOWASSA NA WARAKA WA KOMBA
Jumatano wiki hii, kupitia vyombo vya habari, Lowassa alisambaza waraka mzito wa kumlilia Kapteni Komba ambapo mbali na maneno mengine aliandika:“Hivi ni kweli sitasikia tena sauti yako Kapteni Komba! Mbona umeondoka bila kuniaga ndugu yangu! Moyo wangu unabubujika machozi ya damu.
“Kapteni Komba, mimi na wewe tumepigana vita nyingi kwa maslahi ya chama na nchi yetu na kushinda vita hivyo. Lakini bado tulikuwa tunaendelea na mapambano ya kumnasua Mtanzania kutoka katika umaskini.”
MSAIDIZI WAKE ANENA
Wakati waraka huo ukiendelea kuwa gumzo kutokana na kuwagusa watu wengi, Uwazi Mizengwe liliwasiliana na msaidizi wa Lowassa, Abubakari Liongo ili kupata ufafanuzi wa taarifa za huzuni ya kiongozi wake inayomtokea mara kwa mara.
“Tunashukuru kwa sapoti tunayopata kutoka kwa wananchi lakini kusema kweli mzee yuko kwenye wakati mgumu, nafikiri ni kwa sababu anawapenda watu wake na asingependa kumpoteza hata mmoja mpaka safari yake ya matumaini kwa Watanzania (hakufafanua) itakapotimia.
WIMBO WA KOMBA KWA LOWASSA
Saa chache kabla ya kifo cha Kapteni Komba, habari zinaeleza kuwa mbunge huyo wa Mbinga Magharibi alimuandikia wimbo Lowassa wa kumsapoti kwenye mbio zake za urais akiamini kuwa waziri mkuu huyo wa zamani ndiye atakayeshinda kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuwa mgombea urais mwenye matumaini ya kushinda katika uchaguzi mkuu ujao.
Wimbo huo ulikuwa na kiitikio:
“Jembe ni nani?
Huyu, huyu, huyu huyu anatufaa
Ni nani huyooo?
Huyu, huyu X3 Anatufaa
Jembe ni nani huyo?
Jembe ni Lowassa.
Lowassa anatajwa kuwania urais mwaka huu kuchukua mikoba ya mwanamtandao mwenzake, Rais Jakaya Kikwete ambaye wakati anaingia ikulu alitajwa kuwa ni pacha wake kiasi cha wawili hao kupewa jina la utani la Boys II Men, wakifananishwa na wasanii wa kundi mahiri la muziki laini la nchini Marekani.
Subscribe to:
Post Comments
(Atom)
TOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO

Find us on Facebook
Popular Posts
My Blog List
-
DKT. HUSSEIN OMAR AIPONGEZA TET KATIKA JITIHADA ZA KUKUZA SEKTA YA ELIMU NCHINI. - -Avutiwa na Utendaji katika Mifumo ya TEHAMA NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Hussein Mohamed Omar ameipongeza Taasisi ya El...35 minutes ago
-
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ASHIRIKI KIKAO CHA KIMATAIFA CHA SHERIA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI - Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari ameshiriki kikao cha 58 cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Sheria za Biashara na Uwekezaji kinachofanyi...1 hour ago
-
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ASHIRIKI KIKAO CHA KIMATAIFA CHA SHERIA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI - Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari ameshiriki kikao cha 58 cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Sheria za Biashara na Uwekezaji kinachofanyi...1 hour ago
-
NBC Yakutana na Wateja Wake Wakubwa wa Jijini Arusha, Yajadili Fursa, Ufanisi wa Huduma Zake Kwa wateja. - Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekutana na wateja wake wakubwa kutoka kampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) wa jijini Arusha ili k...16 hours ago
-
Biashara : NBC Yakutana na Wateja Wake Wakubwa wa Jijini Arusha - Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekutana na wateja wake wakubwa kutoka kampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) wa jijini Arusha il...16 hours ago
-
Why are Japanese Cars so popular in the Arab World - Japanese cars have firmly established their presence in Arab markets, becoming a symbol of quality and reliability. The continued demand for these vehicl...5 days ago
-
สมัคร wing888 VIP เว็บตรงคุณภาพสูง และบริการคุณภาพ - Wing888 vip เป็นหนึ่งในชื่อที่น่าสนใจโดยเฉพาะสำหรับผู้ที่ให้ความสำคัญกับความปลอดภัย เสถียรภาพ และระบบการให้บริการที่จริงจัง ความเป็นส่วนตัวและความซื่อสัตย...2 months ago
-
BENKI YA STANBIC YAFIKIA TAMATI KAMPENI YA TAP KIBINGWA KWA SHANGWE - • TZS milioni 7.5 zimetolewa kama zawadi kwa wateja 15 waliotumia Visa Debit Card zao kwa miezi mitatu • Washindi wengine watano wajishindia TZS 500...3 months ago
-
KIWANJA CHA NDEGE SUMBAWANGA CHAFIKIA ASILIMIA SITINI YA UJENZI. - Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga umefikia asilimia sitini ya utekelezaji wake. Taarifa hiyo imetolewa mbele waandishi wa habari leo Machi 26, 20...3 months ago
-
Majina ya Blog Zinazoanzia na Herufi ya V - *1. VOA Sauti ya America * www.voaswahili.com *2. Vijimambo* lukemusicfactory.blogspot.com4 months ago
-
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025 - Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini ke...4 months ago
-
ZANZIBAR: UBALOZI WA NORWAY TANZANIA WAIPONGEZA TAMWA-ZNZ UTEKELEZAJI MRADI WA SWIL. - *Maafisa Ubalozi wa Norway wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TAMWA-ZNZ mara baada ya kumaliza mazungumzo katika ofisi zilizopo Tu...3 years ago
-
AUDIO | Harmonize - Kushoto Kulia | Download - *DOWNLOAD* Listen to Harmonize - Kushoto Kulia byDJ Mwanga on hearthis.at5 years ago
-
-
Ufafanuzi wa TCRA kuhusu kuondoa chaneli za runinga zinazotazamwa bila kulipia (FTA) kutoka ving'amuzi vya Azam, Multichoice na Zuku - Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imefafanua kuhusu kuondoa Channel za Televisheni za ndani zinazotazamwa bila kulipia (FTA) kutoka Ving’amuzi vya Azam, Multic...6 years ago
-
MSANII ROSE MUHANDO: SIOGOPI WANAONISEMA VIBAYA - Rose Muhando. STAA wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amefunguka kuwa, haogopi watu wanaomsema kwa ubaya kila kona bali anaangalia kile kilichomsababisha ku...8 years ago
-
VIDEO: SNURA AONGELEA KUFANYA KAZI NA DON JAZZY..! - Kila mtu alilipokea kwa style yake hili suala la mtayarishaji na msanii mkubwa wa muziki barani Afrika *Don Jazzy *kujirecord video akiimba wimbo wa Chura ...8 years ago
-
PIKIPIKI YAZUA HOFU BAADA YA KUTELEKEZWA MWAKA MZIMA JIJINI DAR ES SALAAM, UKIIKARIBIA, IKIIGUSA INAJIWASHA POLISI WAGWAYA KUIPELEKA KITUONI - Mwananchi akipita kwa kuikwepa pikipiki yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika Kituo cha waendesha...8 years ago
-
-
MATUKIO MBALI MBALI YA ZIARA YA KAMPENI ZA MGOMBEA URAIS WA UKAWA KUPITIA CHADEMA KATIKA JIMBO LA HAI, MKOANI KILIMANJARO - *Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokelewa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai ...9 years ago
-
Bunge Lamkingia Kifua Zitto Kabwe......Lasema Bado ni Mbunge Halali na Spika wa Bunge ana Mamlaka Kisheria Ya Kutengua Maamuzi ya CHADEMA - Ofisi ya Bunge imesema haijapata barua yoyote kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema). Kauli ya hiyo ya Bunge im...10 years ago
-
MAPACHA 6 WALIOZALIWA MWAKA 1983 NCHINI UINGEREZA SASA NI WAKUBWA NA WAMENZA KUWA NA FAMILIA ZAO - * Bwana Na Bibi Grahan Walton wakiwa na mabinti wao sita pamoja na mjukuu wao* * Mapacha hao wa kike wakati wana miaka mitano (Kushoto kwenda kilia) Luci...10 years ago
-
New Song WAKAZI-BIGGIE - Download Here - *Wimbo mpya kutoka kwa Wakazi - Biggie* www.aloyson.com10 years ago
-
-
-
-
-
-
-
-
0 comments:
Post a Comment