Friday, April 3, 2015


HATIMAYE tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC)imetanga rasmi kuhairisha kura maoni ya kupigia Katiba inayopendekezwa na Bunge maalum la Katiba ambayo ilitarajiwa kufanyika tarehe 30 Aprili mwaka huu mpaka pale watakapotangaza tarehe maalum.AnaandikaKAROLI VINSENT.endelea nayoKutokana na Tume hiyo kushindwa kumaliza kuwaandisha kwa wakati wananchi kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo mpya wa Biometric Voters Regislation,(BVR). nchi nzima kwa mwezi mmoja uliobaki.Akitangaza kuhairisha zoezi hilo mda huu jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Jaji Mstaafu Damiani Lubuva wakati wa Mkutano na vyombo vya Habari ambapo amesema tume hiyo imefikia maamuzi ya kuhairisha kura ya maoni kutokana na sababu zilizojitokeza kwenye uandikishaji Mkoani njombe.
“Kwa vile zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura halijakamilika,tume haitaweza kuendelea na zoezi la upigaji kura ya maoni,hivyo zoezi hilo lilitangaza awali la kura ya maoni
kufanyika tarehe 30 aprili limehairishwa hadi tarehe itakayotangazwa na NEC”amesema Jaji Lubuva
Jaji Lubuva ameongeza kuwa kutangazwa kwa tarehe husika kutategemea maushauriano na tume ya uchaguzi wa taifa ya Zanzibar (ZEC).
Aidha,Jaji huyo amesema kuwa kutokana na uhaba wa vifaa vya kuwaandikisha wananchi kuwa vichache tume hiyo imeshalipia vifaa vingine ambapo kwa mujibu wa jaji huyo amesema Shehena ya Vifaa vinatajiwa kuwasili kwa awamu tatu kwaanzia sasa.
“Kwa hali tulioishudia mkoani Njombe ambapo tulikuwa na mashine 250 kwa sasa tumeona kuagiza vifaa vingi ili tuweze kuwaandisha wananchi kwa haraka zaidi kwani vifaa vitakuja kwa awamu tano ambayo kwa sasa zinakuja mashine 268 baadae zitakuja mashine 1600 na ya mwisho 1600”ameendelea kusema Jaji Lubuva’
Jaji lubuva amebainisha kuwa vifaa hivyo vikija vyote zoezi zima la kuwaandisha wapiga kura litakamilika nchi nzima mwezi wa Julai.
Vilevile Jaji lubuva amesema kwa sasa serikali imeshalipa gharaza zote za mashine ambazo anasema zimagharimu Dolla milioni 72. 
Kuhusu kuaomba mashine za BVR nje ya nchi.
Jaji lubuva amesema ni kweli tume hiyo ilikwenda nchi hizo na kuomba mashine hizo na kudai hilo ni jambo la kawaida kwani ni nchi rafiki.


Kuibuka huko kwa tume ya uchaguzi NEC inakuja ikiwa tayari wanasiasa mbalimbali wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Demokrasia maendeleo Chadema Freeman Mbowe kupinga zoezi hilo kwa mfumo wa BVR kusema ni vigumu kufanyika kwa wakati.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

TOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO

TOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO

Find us on Facebook

Popular Posts

My Blog List

Total Pageviews

25890

Tweets

NETWORKED BLOGS

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
widgets