Friday, April 3, 2015

Takriban watu 15 wanaodaiwa kufunika nyuso zao wameshambulia chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya.
Watu hao wanadaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri.
Kufuatia shambulizi la chuo kikuu cha Garissa ,Shirika la msalaba mwekundu Red Cross limewataka raia wa Garissa kutoa msaada wa damu.
Walioitikia wito huo tayari wameeleka katika hospitali kuu ya Garissa mbapo kituo cha kutoa damu kimeanzishwa chini ya mti.


Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa Collins Wetangula amesema kuwa wakati wapiganaji hao walipoingia katika nyumba anayolala aliwasikia wakifungua milango na kuwauliza watu iwapo ni waislamu amawakristo.
''Kama wewe ni mkristo unapigwa risasi papo hapo.Kila mlio wa risasi nilipousikia nilidhani nitauawa'',ameliambia shirika la habari la AP.


esema kwamba maafisa wa usalama baadaye waliingia kupitia dirisha moja na kumtoa yeye na wenzake hadi katika eneo salama.




Mwandishi wa habari wa Kenya Dennis Okari ambaye yuko katika eneo la chuo kikuu cha Garissa ameandika katika mtandao wake wa Twitter akisema kuwa:


Wapiganaji hao wako katika jumba la kulala wanafunzi .''Ninaweza kusikia milio ya risasi kutoka upande wa pili.@ntvkenya".

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

TOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO

TOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO

Find us on Facebook

Popular Posts

My Blog List

Total Pageviews

25864

Tweets

NETWORKED BLOGS

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
widgets