Wednesday, May 28, 2014
2:25 PM
| Posted by
Unknown
|

Kwa nyakati tofauti wataalamu hao wa masuala ya afya wamesema dawa hizo ambazo zimekuwa zikitumika kupaka mwilini kama mafuta na matumizi yake kuongezeka zaidi wakati huu kutokana na tishio la homa ya Dengue, zinaweza kuwa na madhara kwa sababu mbalimbali.
Daktari Kiongozi na Mtaalamu wa Homa ya dengue katika Hospitali ya Mwananyamala, Mrisho Rupinda alisema jana kwamba watumiaji wanapoona madhara ya aina yoyote wanatakiwa kuchukua hadhari hasa kwa wenye mzio (alerge).
Alisema kwa kuwa dawa hizo ni kemikali zinahitaji utaratibu na kwa watoto inahitaji uangalifu mkubwa ambapo ni vyema kuwavalisha nguo ndefu na iwapo kuna mbu wengi dawa hizo ni vyema zikapakwa juu ya nguo.
Alisema kwa kuwa ngozi za watoto bado ni changa na laini si vyema kutumia dawa hizo moja kwa moja kwani zimetengenezwa kwa kemikali zinazoweza kuwa siyo salama kwa ngozi za watoto.
Alisema wenye vidonda wanatakiwa kujihadhari kwa kuhakikisha dawa hizo hazigusi vidonda au sehemu zenye michubuko na inapobidi wapake juu ya nguo, kwa wanawake wavaa nguo fupi ameshauri kuvaa soksi kisha kupaka dawa hiyo juu yake kwa kuwa si lazima iguse ngozi.
“Madhara yanaweza kutokea kwa baadhi ya watu hasa wenye alerge (mzio) na wenye matatizo ya ngozi, ni vyema kuchukua tahadhari. Madhara yanaweza kutokea kwa yeyote na wakati wowote,” alisema Dk Rupita.
Mtaalamu wa afya ambaye ni Ofisa wa Taaluma na Udhibiti wa Magonjwa wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Grace Saguti ameonya matumizi yasiyo sahihi ya dawa hizo za kuzuia mbu mwilini na kusema watumiaji wanatakiwa kupaka kwa kufuata taratibu na si kutumia kiholela.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki, Dk. Saguti alisema japokuwa suala hili ni la kitaalamu zaidi watu wanapaswa kuwa makini kuhusu namna wanavyotumia vizuizi hivyo vya mbu katika miili yao.
“Vizuizi hivyo vinaweza kuwa na reaction kutokana na mwili wa mtu. Sitalizungumzia kwa undani zaidi kwa kuwa kila kitu kina madhara yake lakini watu wasikimbilie kutumia dawa hizo bila kupata ushauri. Ninajua iwapo mtu atakuwa na vidonda si vyema kutumia dawa hizo bila kufuata maelekezo kwa usahihi,” alisema.
Kwa mujibu wa Dk. Saguti, suala hilo la matumizi linahitaji pia tahadhari na kufuata maelekezo ikiwamo kuhakikisha mwili unakuwa safi wakati wa kupaka dawa hizo ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kwenye ngozi.
Matumizi ya dawa hizo yameshika kasi katika maeneo mengi nchini kwa sasa hasa kutokana na tishio la ugonjwa wa dengue unaoenezwa na mbu aina ya Aedes Egyptiae ambao mara nyingi huuma wakati wa mchana.
Subscribe to:
Post Comments
(Atom)
TOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO

Find us on Facebook
Popular Posts
Widget by Making Different
My Blog List
-
WANYARWANDA WAADHIMISHA MIAKA 31 TANGU KUTOKEA KWA MAUAJI YA KIMBARI, WAHIMIZWA KUTUNZA HISTORIA - Waziri wa Katiba na Sheria, Damas Ndumbaro akiwasha mshmaa leo Aprili 07, 2025 jijini Dar es Salaam katika kumbukizi ya miaka 31 ya mauaji ya kimbari ...3 minutes ago
-
WANYARWANDA WAADHIMISHA MIAKA 31 TANGU KUTOKEA KWA MAUAJI YA KIMBARI, WAHIMIZWA KUTUNZA HISTORIA - Waziri wa Katiba na Sheria, Damas Ndumbaro akiwasha mshmaa leo Aprili 07, 2025 jijini Dar es Salaam katika kumbukizi ya miaka 31 ya mauaji ya kimbari yal...5 minutes ago
-
DKT. MPANGO MGENI RASMI UTOAJI WA TUZO ZA MWALIMU NYERERE UANDISHI BUNIFU - NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Utoaji ...2 hours ago
-
Siasa : Balozi Nchimbi atoa wito, Uchaguzi wa 2025 - Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema kuwa msingi wa sera za CCM utabakia kuwa ni maendeleo ya watu pamoja...8 hours ago
-
KIA Sportage R Review: Specs, Features, and Performance Breakdown - The KIA Sportage R, produced from 2010 to 2015, is a compact SUV known for its stylish design, improved ride quality, and modern features. With KIA’s sig...5 days ago
-
NELSON MANDELA NA TMA KUWAJENGEA UWEZO WATAALAMU WA HALI YA HEWA KUPITIA TEKNOLOJIA YA AKILI MNEMBA - Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali y...5 days ago
-
KIWANJA CHA NDEGE SUMBAWANGA CHAFIKIA ASILIMIA SITINI YA UJENZI. - Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga umefikia asilimia sitini ya utekelezaji wake. Taarifa hiyo imetolewa mbele waandishi wa habari leo Machi 26, 20...1 week ago
-
Majina ya Blog Zinazoanzia na Herufi ya V - *1. VOA Sauti ya America * www.voaswahili.com *2. Vijimambo* lukemusicfactory.blogspot.com4 weeks ago
-
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025 - Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini ke...5 weeks ago
-
Dog House Megaways: Slot Gacor dengan Kemenangan Besar - Pendahuluan Dog House Megaways dari Pragmatic Play adalah salah satu game slot online gacor yang populer di kalangan pemain karena fitur Megaways yang me...5 months ago
-
ZANZIBAR: UBALOZI WA NORWAY TANZANIA WAIPONGEZA TAMWA-ZNZ UTEKELEZAJI MRADI WA SWIL. - *Maafisa Ubalozi wa Norway wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TAMWA-ZNZ mara baada ya kumaliza mazungumzo katika ofisi zilizopo Tu...2 years ago
-
AUDIO | Harmonize - Kushoto Kulia | Download - *DOWNLOAD* Listen to Harmonize - Kushoto Kulia byDJ Mwanga on hearthis.at5 years ago
-
-
Ufafanuzi wa TCRA kuhusu kuondoa chaneli za runinga zinazotazamwa bila kulipia (FTA) kutoka ving'amuzi vya Azam, Multichoice na Zuku - Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imefafanua kuhusu kuondoa Channel za Televisheni za ndani zinazotazamwa bila kulipia (FTA) kutoka Ving’amuzi vya Azam, Multic...6 years ago
-
KAMPUNI YA ORYX GAS YAJIVUNIA KUWA RAFIKI WA MAZINGIRA - Na Emmanuel Masaka,Dar. KAMPUNI ya mama katika usambazaji na uuzaji wa gesi ya ORYX nchini ijulikanayo kama ORYX ENERGIES LTD imekuwa mstari wa mbe...6 years ago
-
MSANII ROSE MUHANDO: SIOGOPI WANAONISEMA VIBAYA - Rose Muhando. STAA wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amefunguka kuwa, haogopi watu wanaomsema kwa ubaya kila kona bali anaangalia kile kilichomsababisha ku...7 years ago
-
PIKIPIKI YAZUA HOFU BAADA YA KUTELEKEZWA MWAKA MZIMA JIJINI DAR ES SALAAM, UKIIKARIBIA, IKIIGUSA INAJIWASHA POLISI WAGWAYA KUIPELEKA KITUONI - Mwananchi akipita kwa kuikwepa pikipiki yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika Kituo cha waendesha...8 years ago
-
-
MATUKIO MBALI MBALI YA ZIARA YA KAMPENI ZA MGOMBEA URAIS WA UKAWA KUPITIA CHADEMA KATIKA JIMBO LA HAI, MKOANI KILIMANJARO - *Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokelewa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai ...9 years ago
-
Bunge Lamkingia Kifua Zitto Kabwe......Lasema Bado ni Mbunge Halali na Spika wa Bunge ana Mamlaka Kisheria Ya Kutengua Maamuzi ya CHADEMA - Ofisi ya Bunge imesema haijapata barua yoyote kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema). Kauli ya hiyo ya Bunge im...10 years ago
-
MAPACHA 6 WALIOZALIWA MWAKA 1983 NCHINI UINGEREZA SASA NI WAKUBWA NA WAMENZA KUWA NA FAMILIA ZAO - * Bwana Na Bibi Grahan Walton wakiwa na mabinti wao sita pamoja na mjukuu wao* * Mapacha hao wa kike wakati wana miaka mitano (Kushoto kwenda kilia) Luci...10 years ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Total Pageviews
25962
0 comments:
Post a Comment